Hadija Mwanamboka Aibuka na Vitu Vvya Hadija Kinondoni Blok 41
Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini, Khadija Mwanamboka amesema ubunifu anaoutumia kwenye mavazi, aliuhamishia kwenye biashara yake ya mgahawa wa vyakula ‘VVK’ ndio maana mwezi huu unatimiza mwaka mmoja ukiwa na mafanikio makubwa. Khadija ameeleza kuwa kupitia mgahawa huo wa VVK ambacho ni kirefu cha Vitu Vya Khadija uliopo Block 41 Kinondani, jijini Dar es salaam, amesema dani ya mwaka mmoja ameweza kuvuka matarajio ya kuwafikia wateja wengi zaidi.





