Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini, Khadija Mwanamboka amesema ubunifu anaoutumia kwenye mavazi, aliuhamishia kwenye biashara yake ya mgahawa wa vyakula ‘VVK’ ndio maana mwezi huu unatimiza mwaka mmoja ukiwa na mafanikio makubwa. Khadija ameeleza kuwa kupitia mgahawa huo wa VVK ambacho ni kirefu cha Vitu Vya Khadija uliopo Block 41 Kinondani, jijini Dar es salaam, amesema dani ya mwaka mmoja ameweza kuvuka matarajio ya kuwafikia wateja wengi zaidi.

“Nimeamua kuwa serious kwenye hii restaurant kwa sababu wateja wetu wamekubali huduma zetu. Mimi kama mbunifu wa mavazi kuingia kwenye sekta ya chakula haikuwa ngeni. Mimi ni mbunifu wa mavazi kwahiyo nilihamisha ule ubunifu wangu kwenye upande wa chakula,” amesema.
Basicaly hata chakula ninachouza ni chakula ambacho hata mimi nakipenda. Ni chakula ambacho mimi najua kukipika,” ameongeza.

Khadija anasema baada ya kuweza kuwafikia wateja wao wengi ndani ya mwaka mmoja, sasa wamejipanga kutoa ofa nyingi kwa wafanyakazi wa maofisini.

“Tuna plan kubwa sana ya kuboresha huduma,” anasema.

“Tunataka kuwa na ofisi ambazo zitakuwa VVK members. Kwa mfano labda kwenye ofisini kuna watu 15 wamejisajiri, watu hao watapata chakula kwa nusu ya bei, kama mfano biriani ni shilingi 10,000, wao watapata kwa shilingi 5,000 kila siku. Mungu akipenda utaratibu huu utaanza mwezi wa pili lakini kwa kipindi hiki wanaweza kuendelea kupata huduma zetu za kila siku na baadaye tutawatangania kwa kutumia mitandao yetu ya kijamii pamoja na tovuti yetu.”

Pia Khadija amesema wanatoa huduma za chakula kwenye sherehe mbalimbali pamoja na kutoa ushauri.

Mwanamitindo mahiri nchini Khadija Mwanamboka, amefungua kiota kipya kabisa maeneo ya Kinondoni Blok 41 kinachotoa huduma ya mambo ya maakuli na vinywaji laini, ikiwa ni pamoja na Juice fresh za matunda mbalimbali kama Embe. Pasion, Nanasi, Fenesi, na mengineyo mchanganyiko, pamoja na vyakula vya aina mbalimbali vinavyopatikana kwa mtindo wa Bufee. Eti ni 'VITU VYA KHADIJA' fika ukajionee mwenyewe Vitu vya Hadija, Kiota hicho kimefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ramani ya kufika kiotani ni, ukitokea barabara kubwa ya Kinondoni maeneo ya Biafra unakata kushoto, kona ya kwanza kushoto kwako tena unanyoola utakutana na kibao hiki, pia unaweza kutokea nyuma ya jengo la Airtel Morocco

Mandhari ya ndani ya kiota hicho ni kama hivi meza na viti vyote ni rangi pendwa.....

Mandhari ya kiotani

Menu ya huduma zinazopatikana mahala hapo.

Pia ukifika hapo utapata vitu kama hivi ndani ya Supermarket iliyopo kiotani hapo

Ndani ya Supermarket

Ufuta...na vinginevyo